Step 2 of 3 / Accept terms
Terms and Conditions
Please read the apartment terms once. After accepting, the selected apartment will be carried into the payment form automatically.
Rickie Apartments - Mkwajuni Monduli
Mkwajuni, Vijibweni, Kigamboni / TZS 300,000 per monthly / Minimum 6 months
Apartment contract terms
These terms are maintained by the administrator for this apartment. Minimum payment is 6 months and maximum is 9 months.
1. Mpangaji atalipa kodi kamili kwa kipindi chote cha upangaji kilichokubaliwa katika mkataba.
2. Mpangaji atawajibika kudumisha usafi ndani na nje ya chumba au nyumba anayoishi.
3. Mpangaji atatunza vifaa vyote vya nyumba, ikiwemo milango, vitasa, madirisha, mfumo wa umeme, rangi na vifaa vingine vilivyowekwa katika chumba au nyumba.
4. Mpangaji atalipa bili za umeme na maji kwa wakati katika kipindi chote cha mkataba.
5. Kuchelewesha malipo ya bili ya maji kutasababisha adhabu ya TZS 15,000 kwa mujibu wa utaratibu wa DAWASA.
6. Mpangaji atawajibika kulipa gharama za kurekebisha au kubadilisha mali yoyote atakayoharibu ndani au nje ya chumba/nyumba, isipokuwa uharibifu unaotokana na uchakavu wa kawaida.
7. Endapo mpangaji ataamua kuondoka kabla ya kipindi cha mkataba kumalizika, kodi au gharama nyingine alizolipa hazitarejeshwa.
8. Endapo mpangaji atakiuka masharti ya mkataba au kusababisha matatizo kwa wapangaji wengine, mwenye nyumba atakuwa na haki ya kusitisha mkataba. Kodi iliyobaki inaweza kurejeshwa baada ya kukokotoa muda aliokaa mpangaji pamoja na makato ya madeni, uharibifu au gharama nyingine anazodaiwa.
9. Mpangaji atatoa taarifa kwa mwenye nyumba angalau mwezi mmoja kabla ya mkataba kumalizika, akieleza kama anataka kuhuisha mkataba au kuondoka.
10. Mpangaji atatumia chumba au nyumba kwa madhumuni ya makazi pekee.
11. Mpangaji haruhusiwi kumpangisha mtu mwingine chumba/nyumba yote au sehemu yake bila kibali cha maandishi kutoka kwa mwenye nyumba.
12. Mpangaji atawajibika kushiriki au kugharamia uondoaji wa majitaka endapo shimo la majitaka litajaa, kwa mujibu wa utaratibu wa nyumba au makubaliano na mwenye nyumba.
13. Mpangaji haruhusiwi kufulia nguo ndani ya choo au bafu, isipokuwa kama eneo hilo limetengwa au kuruhusiwa kwa matumizi hayo.